Skip to content Skip to footer

KUTATUA SHIDA YA WATEJA WA CHELEWAJI – HANDLING TARDY CLIENTS

Wachelewaji siku zote wawekee ratiba za mwisho kabisa. Itakusaidia kuweka msimamo wa nidhamu katika kutatua shida ya wateja wa chelewaji.

Hata kama utafanya kila jambo ndani ya uwezo wako kuzungumza / kuwasiliana ipasavyo.. Upo wakati utakutana na nyakati zinazo chefua hali ya hewa (kuzidi uwezo wako).

Jinsi utakavyo pokea hali hiyo kwa uwezo wako wa kuwasiliana uso kwa uso na changamoto ni kitendawili kufanikiwa kati kati ya watu wa taaluma.

Sijui kama unanielewa? Hebu rudia kuisoma hii point utaelewa zaidi.. Kutatua Shida Ya Wateja wachelewaji.

HANDLING TARDY CLIENTS.

Kwa sababu wana taaluma ya urembo hutegemea ratiba kutoka kwao wateja ili kupangilia muda wa kazi husika. Sasa mteja mwenye kasumba ya uchelewaji husababisha matatizo kabisa.

Mteja mmoja akichelewa ratiba yake, basi ameharibu ratiba (Appointments) za siku nzima hata kwa wateja wengine.

Ushauri: Sio vizuri kuchelewa ratiba yako ya Salon. Utaleta mafarakano na kuharibu hali ya hewa (mood) Cha kufanya: Zingatia muda na timiza ahadi yako.

MIONGOZO MICHACHE YA KUTATUA SHIDA YA WATEJA WACHELEWAJI NI KAMA IFUATAVYO;

1- kubaliana na utaratibu wa Salon 2- Hatarisha ratiba zingine upone 3- Wajue wateja wako wachelewaji 4- Mapokezi wapige simu kisha wa kujuze.

USISAHAU KWAMBA UNAHITAHIJI PESA

Fuafuta kidogo haya maelekezo ya jinsi gani ya kutatua Shida ya wateja wachelewaji
1- Fahamu na kukubaliana na utaratibu wa Salon wa kuweka ratiba (Appointment)..

Salon nyingi wenye uelewa wa nini maana ya kuwa utaratibu wa Appointment (ratiba) kipindi mteja anahitaji kuja Salon kupata huduma..
huweka kikomo kwa muda unao ruhusiwa endepo utachelewa kabla ya ratiba na kwamba itakubidi uweke ratiba upya…

Mara nyingi wateja wakichelewa zaidi ya dakika 15 wanatakiwa kurudia kuweka ratiba zao upya tena kwa siku yenye nafasi…

Faida sahihi; wateja wengi watakubali na kuelewa kuhusu huo utaratibu, lakini utakutana na wateja wachache wanao lazimisha kuhudumiwa upesi..

Sasa utafanyaje?

(a) Waeleweshe kwamba, unaratiba na watu wengine pia wana haraka zao na wamezingatia muda vizuri.

(b) Waeleweshe Kwamba, kuharakisha ndani ya kutoa huduma hairuhusiwi kazini hata katika kutoa huduma kwako wewe mteja wetu.
2- Kama mteja mchelewaji kafika na una muda wa kumuhudumia, hatarisha ratiba zingine..
mjulishe kwa nini wampatia huduma hata kama amechelewa.
Mweleze wazi taarifa kidiplomasia uendelee na kazi..

3- Unavyo zidi kuwafahamu wateja, utajua mwenye tabia ya kuchelewa ni yupi! +Wachelewaji siku zote wawekee ratiba za mwisho kabisa..

4- Kama muda Una yoyoma mwambie mapokezi wampigie simu mteja kisha wakujuze.

Uchelewaji husababisha saratani ya matatizo, hivyo epuka kuchelewa nenda na wakati itakuondolea kero za hapa na pale..

hapa bigwayssalon.com tunao utaratibu wa kuweka APPOINTMENT (ratiba) kumuondolea usumbufu na kuongeza heshima kwako mteja na kwa kazi yetu kama wana taaluma ya urembo wa nywele, kucha na uangalizi wa ngozi.

Kama umejifunza kitu tafadhali tuambie changamoto gani imekutatiza muda mrefu na unatamani kuondokana nayo hasa kwa upande wa sanaa ya urembo..

Tutakusaidia uweze kushinda hiyo shida.. Karibuni sana..hapa kwetu tunasema kwamba ni nywele na tamaduni ya urembo. Tukutane kwa post zinazofuata.

Endelea KUTUFUATILIA.

Leave a comment